Chanzo cha picha, Getty Images
Iran imeitaka
Israel kusitisha mara moja mashambulizi yake kusini mwa Lebanon, ikitishia
kutoa “kujibu vikali” iwapo uvunjifu wa makubaliano ya kusitisha
mapigano utaendelea.
Makao makuu
ya jeshi mjini Tehran yamesema Israel imekiuka makubaliano hayo mara 84 katika
kipindi cha siku mbili zilizopita.
Kwa upande
mwingine, Rais wa Marekani Donald Trump ametoa kauli nzito akikosoa mbinu za
kivita za Israel dhidi ya Hezbollah.
Rais Trump
ameeleza kutoridhishwa na kitendo cha Israel kubomoa majengo ya ghorofa kwa
ajili ya kutafuta mtu mmoja, akisisitiza kuwa raia wengi wanaopoteza maisha si
wapiganaji wa Hezbollah.
“Ikiwa
Israel haiwezi kufanya operesheni yake bila kuua kila mtu, basi Syria itafanya
kazi hiyo,” Trump alisema.
Katika
pendekezo la kushangaza, Rais Trump amedokeza kuwa ni bora kuiachia Syria
jukumu la kushughulikia kundi la Hezbollah, akiamini kuwa inaweza kufanya kazi
hiyo kwa ufanisi zaidi bila kusababisha vifo vingi vya raia.
Shinikizo la
kimataifa dhidi ya operesheni za kijeshi za Israel limefikia kilele huku kukiwa
na mgogoro wa kidiplomasia kuhusu hatua za kijeshi nchini Lebanon na Gaza.