Meli za mafuta za Iran zimevuka eneo la kizuizi cha Marekani kuzunguka bandari za Iran, ambazo zilikuwa zimetia nang hapo kwa takriban miezi miwili, tovuti ya ufuatiliaji wa baharini ya TankerTrackers imeripoti Jumatano, Juni 17, kabla ya kusainiwa kwa makubaliano kati ya Tehran na Washington yaliyopangwa kufanyika Ijumaa. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Angalau meli mbili kubwa za mafuta za shirika la umma la kusafirisha mafuta la Iran (NITC), zinazoitwa Diona na Hero2, zilivuka eneo la kizuizi cha Jeshi la Wanamaji la Marekani, zikiwa zimebeba jumla ya mapipa milioni 3.8 ya mafuta ghafi ya Iran,” tovuti hiyo imesema kwenye mtandao wa kijamii wa X, baadaye ikiripoti kupitishwa kwa meli ya tatu ya mafuta ya Iran. “Haya ni mauzo ya kwanza ya mafuta ghafi ya Iran katika kipindi cha miezi miwili,” imebainisha.

Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif alitangaza siku ya Jumapili, Juni 14, 2026, kwamba Marekani na Iran zimefikia makubaliano ya amani. Mkataba wa makubaliano ulisainiwa kwa njia ya video siku ya Jumatatu, Juni 15, lakini sherehe imepangwa kufanyika siku ya Ijumaa, Juni 19, nchini Uswisi. Mazungumzo yataendelea tena Ijumaa ili kufikia makubaliano ya mwisho. Mkuu wa timu ya mazungumzo ya Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf, na Makamu wa Rais wa Marekani J.D. Vance watahudhuria sherehe ya kusaini mkataba huu wa makubaliano kati ya Tehran na Washington.

Itifaki ya makubaliano kati ya Iran na Marekani ulisainiwa kwa kupitia njia ya video siku ya Jumatatu, Juni 15. Hata hivyo, utiaji saini huu utafanyika rasmi katika sherehe itakayofanyika siku ya Ijumaa nchini Uswisi, ambayo itahudhuriwa na Makamu wa Rais wa Marekani J.D. Vance na mkuu wa timu ya mazungumzo ya Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf. Maudhui ya makubaliano hayajajulikana rasmi bado, lakini ni mwanzo kabla ya mazungumzo kufikia makubaliano ya mwisho. Donald Trump alisema kwamba Mlango wa Hormuz “utakuwa wazi kabisa” siku ya Ijumaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *