Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa ambayo haijawahi kuwekwa wazi, Cabo Delgado imeshuhudia ongezeko la ukatili wa kingono tangu kuanza kwa mgogoro huo mwaka wa 2017. Eneo hili, lenye utajiri wa malighafi, linakabiliwa na vurugu za kundi la kigaidi la Al Shabab, pamoja na kisasi cha kikatili kutoka kwa Vikosi vya Jeshi vya Msumbiji. Wanawake huathiriwa hasa na hali hii.

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu maalum huko Msumbiji, Gaƫlle Laleix

Hii ni sehemu ya saba ya uchunguzi wa “Mozambique Exposed” uliofanywa na muungano unaoratibiwa na Forbidden Stories, ambapo RFI ilichangia.

Asubuhi ya Machi 2021, karibu saa 11 alfajiri, Olessa Ibrahimou aliamshwa na milio ya risasi. Wanaume wenye silaha waliingia kwa kasi katika kijiji chake, msituni, karibu na mji wa Palma, mji mkuu wa wilaya yenye jina moja nchini Msumbiji. Olessa Ibrahimou na watoto wake watano walijaribu kukimbia lakini waliangukia mikononi mwa washambuliaji. “Waliwatenganisha watoto na watu wazima,” anakumbuka mwanamke huyu mwenye umri wa miaka 41aliyekondieana sana. “Waliponiona, watoto zangu watatu wadogo  walinikimbilia. Majambazi walitutenganisha kwa sababu nilikuwa mjamzito. Lakini waliwachukua binti zangu wawili, wenye umri wa miaka 15 na 17.”

Tangu siku hiyo, Olessa Ibrahimou hajawahi kuwaona binti zake tena. Sasa anaishi Pemba, mji mkuu wa Cabo Delgado, katika umaskini mkubwa. “Nilimpata jirani ambaye alitekwa nyara na kufanikiwa kutoroka,” anaongeza. “Aliniambia kwamba binti yangu mdogo alizaa na ana mtoto sasa.”

Ripoti ambayo haijachapishwa

Hadithi nyingi kama za Olessa Ibrahimou zinaweza kupatikana katika ripoti ya UNFPA (Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa) kuhusu ukatili wa kijinsia (GBV). Hati hii iliyoandikwa mwaka wa 2024 na yenye kichwa cha habari “Sauti za Msumbiji,” haikuchapishwa kamwe, ikitaja wasiwasi wa “ubora”, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa, ambalo halikutoa maelezo zaidi.

Kati ya mwezi Januari na Aprili 2024, zaidi ya watu mia moja walihojiwa na UNFPA katika wilaya saba kati ya kumi na sita za Cabo Delgado. Eneo hili, lenye utajiri wa malighafi (gesi, mawe ya thamani, lithiamu, n.k.), limekuwa likiteseka kwa karibu miaka kumi kutokana na vurugu za kundi lenye silaha la Al-Shabab, pamoja na ulipizaji kisasi unaofanywa na Vikosi vya Jeshi vya Msumbiji katika vita vyao dhidi ya ugaidi.

Waathiriwa, jamaa, wafanyakazi wa kibinadamu, viongozi wa jamii, na watu mashuhuri wa kidini waliohojiwa na shirika la Umoja wa Mataifa wanakubaliana kuhusu jambo moja: tangu mwanzo wa mgogoro mwaka wa 2017, eneo hilo limepitia ongezeko la unyanyasaji wa kijinsia.

Wanawake waliotekwa nyara hubeba vifaa vya wapiganaji, hupika, na kukusanya kuni. Baadhi pia huwa watumwa wa kingono wa magaidi. “Walipotaka kutuadhibu, walitufunga mikono nyuma ya migongo yetu na kutuacha hivyo kwa siku tatu. Wakati huo, mwanaume yeyote aliyetaka angeweza kuja na kutubaka,” mwathiriwa mmoja aliiambia UNFPA.

Manusura wanapofanikiwa kutoroka, mara nyingi wanakabiliwa na unyanyapaa wa jamii zao. “Katika miji ambayo imekaliwa na magaidi, kama vile Palma au Mocimboa da Praia, wanawake wajawazito wanaweza kubaguliwa na jamii zinazoshuku kwamba baba wa mtoto ni mpiganaji,” anaelezea mtaalamu wa masula ya unyanyasaji wa kijinsia katika UNFPA.

Uhalifu na matumizi mabaya ya madaraka

Vile vile, ripoti ya Umoja wa Mataifa inaonyesha kwamba Vikosi vya Wanajeshi vya Msumbiji (FADM) vinahusika na mashambulizi mengi ya kingono. Visa vingi vya  kingono na ubakaji vinaripotiwa. “Jana, afisa alimpa msichana wa miaka 15 au 16 kinywaji,” chanzo kimoja katika Umoja wa Mataifa kilisimulia. Baadae alidai alimpe. Kwa kuwa msichana huyo hakuwa na pesa, alimlazimisha kulala naye. Kuna hoteli karibu. Msicahan huyo alisikika akipiga kelele na kulia.

Kulingana na mashahidi kadhaa waliohojiwa kwenye tovuti na RFI, FADM hutumia vibaya mamlaka yao mara kwa mara. “Hawana heshima,” anasema Saviana Talessa, rais wa kamati ya afya ya kitongoji cha Mocimbao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *