#HABARI: Chini ya Rais Dkt. Samia Mradi wa ujenzi wa stendi mpya ya mabasi Jijini Arusha (Bondeni City) ni sehemu ya mpango wa TACTIC-Masoko unaotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kushirikiana na Serikali Kuu na Mfuko wa Dunia (World Bank), ukiwa na gharama ya jumla ya takribani shilingi 51,561,584,300 sawa na takribani dola za Marekani 21,006,406, ambapo sehemu ya stendi na uwanja wa malori
pekee inakadiriwa kugharimu shilingi 28,149,493,740 sawa na
takribani dola 11,472,251.

Ujenzi huu ulitarajiwa kuanza Juni 2025 na kuchukua miezi 18 hadi 24 kukamilika hivyo kukadiriwa kumalizika Mei 2026, na hadi sasa ripoti zinaonyesha utekelezaji umefikia takribani asilimia 6; mradi unatarajiwa kuunda ajira 350 hadi 500 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja katika hatua ya ujenzi.

Stendi itakuwa na uwezo wa kupokea mabasi 400 kwa siku na itakuwa na bays za kusubiri na kupanda, maeneo ya kusubiri wasafiri, maduka, vyumba vya
kupumzika, ofisi, vyoo, ulinzi kupitia ukuta na CCTV, sehemu ya mafuta na maegesho ya magari; huduma za maji zitapatikana kupitia Arusha Water Supply & Sanitation Authority au visima (boreholes).

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *