Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei amesema maafisa wa Iran wamefanya juhudi kubwa kwa nia njema kufikia makubaliano ya maelewano na Marekani, huku rais wa Marekani akitumia njia mbalimbali za mashinikizo kutokana na kukata tamaa.

“Taifa la Iran lenye hamasi na aminifu, kama mlivyoarifiwa, mkataba wa makubaliano umesainiwa kati ya marais wa Iran na Marekani,” amesema Ayatullah Khamenei katika ujumbe uliotolewa jioni ya jana Alhamisi na kuongeza: “Katika hatua hii, maafisa wa serikali, kwa huruma na nia njema, wamefanya jitihada kubwa, na bila shaka ni rais wa Marekani ambaye, kutokana na kukata tamaa, alikuwa akitumia vipengele mbalimbali vya ushawishi kwa lengo hili.”

Ayatullah Mujtaba Khamenei amesema kwenye ujumbe huo kwamba, awali alikuwa na mtazamo tofauti lakini ameidhinisha makubaliano hayo kutokana na ahadi zilizotolewa na Rais Pezeshkian, ambaye akiwa mkuu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa, ameahidi kwa niaba yake na wenzake, kulinda haki za taifa la Iran na Kambi ya Muqawama.

Rais Pezeshkian pia amesema kwamba hatakubali madai yoyote ya ziada ya Marekani, amesema Kiongozi Muadhamu.

“Kuanzia sasa, sisi – nikimaanisha nyinyi, taifa lenye fahari, na mimi mtumishi wenu mnyenyekevu – tunasubiri kutimizwa masharti yaliyotajwa. Lakini ni dhahiri kwamba mazungumzo ya ana kwa ana yatakayofanyika katika siku zijazo hayatakuwa na maana ya kukubali mtazamo wa adui,” amesisitiza Ayatullah Khamenei.

Ameongeza kusema: “Tunatumai kwamba Swala zilizobarikiwa za Bwana wetu [Imam Mahdi] Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake kutukufu, zitaleta ushindi wa aina zote kwa taifa tukufu la Iran.”

Hati ya wa Makubaliano iliyosainiwa na Rais wa Iran Masoud Pezeshkian, na mwenzake wa Marekani, Donald Trump, inatoa wito wa kukomeshwa uhasama daima katika nyanja zote, kuondolewa mzingiro wa majini wa Marekani ndani ya siku 30, kurejeshwa usafirishaji wa kibiashara kupitia Lango-Bahari la Hormuz, mpango wa ujenzi upya wa Iran wenye thamani ya dola bilioni 300, na kuondolewa vikwazo vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *