#HABARI: Basi la Maning Nice lapinduka na kujeruhi abiria waliokuwa wakisafiri kutoka jijini Dar es Salaam kwenda mkoani Ruvuma, tukio lililomfanya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Mahamoud Banga, kufika haraka eneo la ajali.
Baada ya kukagua eneo hilo, Kamanda Banga alielekea moja kwa moja katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe kwa ajili ya kuwajulia hali na kufuatilia kwa karibu maendeleo ya matibabu ya abiria wote walioumia.
Kufuatia ajali hiyo, Kamanda Banga amewataka madereva kuendelea kuzingatia kwa makini sheria zote za usalama barabarani ili kupunguza ajali zisizokuwa za lazima ambazo zinaweza kuepukika.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi mkoani Njombe linaendelea na uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha kupinduka kwa basi hilo ili kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya uzembe wowote uliokuwepo.
Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITV EXTRA>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
Follow ITV TANZANIA RadioOne Tanzania
Capitalradio Tanzania
(Feed generated with FetchRSS)