
Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, muungano maaskofu wa kanisa Katoliki (CENCO) umepinga mpendekezo ya kuifanyia marekebisho katiba ya Kongo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Uamuzi huu umetolewa baada ya maaskofu hao kuwa na majadiliano ya siku tatu kuhusiana na suala hilo tata.
Lengo kuu la majadiliano yaliongozwa na maaskofu hao ilikuwa ni kufanya maamuzi kuhusu suala hilo la mageuzi ya katiba ya Kongo.
Maaskofu hao walisikiliza maoni kutoka kwa wanasiasa wa upinzani na wale wa upande wa rais Félix Tshisekedi pamoja na wataalam na wasomi wa masuala ya katiba kabla ya kufanya uamuzi wao.
Wanasiasa kutoka mrengo wa Rais wa Kongo Félix Tshisekedi wanaunga mkono mapendekezo ya kuifanyia marekebisho katiba ya nchi.
Upinzani nao unaona kwamba mrengo unaomuunga mkono Rais Tshisekedi unatumia nafasi hiyo ya kufanyia katiba marekebisho kama njia moja ya kumfanya rais Tshisekedi kuendelea kusalia madarakani.
“Hatuoni haja wala dharura au nafasi ya kufanyika kwa mageuzi ya katiba.” ilisema taarifa ya maaskofu hao iliosomwa na katiba wao Mkuu Askofu Donatien Nshole.