Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema jeshi la nchi hiyo “linawapa jeshi la wanamaji silaha za nyuklia”, kulingana na vyombo vya habari vya serikali siku ya Jumatano, na kuongeza kuwa anataka kutengeneza meli za kijeshi za tani 10,000.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Bw. Kim aliyasema hayo siku ya Jumanne mjini Nampo (magharibi) wakati wa hafla ya uzinduzi wa meli ya Choe Hyon, mojawapo ya meli mbili za kivita za tani 5,000 zilizozinduliwa mwaka jana na Korea Kaskazini, kulingana na shirika habari la serikali la KCNA.

“Mpango wa kuwapa wanajeshi wa majini silaha za nyuklia unaendelea kwa ratiba bila kupotoka lengo lililowekwa,” kiongozi huyo alisema wakati wa sherehe hiyo.

“Huu ni mwelekeo wa kimkakati wenye umuhimu mkubwa, kwani utahakikisha kwamba nguvu ya nyuklia ya taifa letu inabaki tayari kufanya operesheni mbalimbali zenye ufanisi,” alisema.

Hapo awali Pyongyang ilisema kwamba Choe Hyon ilikuwa na “silaha zenye nguvu zaidi,” na Bw. Kim alifanya ukaguzi kadhaa mwaka huu, ikiwa ni pamoja na kusimamia jaribio la kombora la meli kutoka kwa chombo hicho mwezi Aprili.

“Baada ya Choe Hyon, hivi karibuni meli ya kivita ya Kang Kon itaanza kufanya kazi. Kisha, tutazindua meli za kivita za kimkakati zenye uzito wa tani 10,000 moja baada ya nyingine,” kiongozi huyo alisema.

Korea Kaskazini inatarajiwa “kutengeneza kila mwaka meli mbili za zenye kiwango cha juu kuliko zile za Choe Hyon,” ikiwemo moja ya tani 10,000, alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *