SHINYANGA: WATOTO wanaolelewa kwenye kituo cha Muvuma Kata ya Nyasubi Halmashauri ya Manispaa ya Kahama wameomba kupatiwa Bima ya Afya na ‘solar’.

Walezi wa kituo hicho, Agata Charles na Evarist Masanja wamesema hayo mbele ya Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania( TRA) Mkoa wa Kikodi Kahama Wisaka Kamwamu alipokuwa ameambatana na baadhi ya watumishi walipokuwa wakikabidhi msaada wa vyakula,vinywaji, sabuni ikiwemo Sh 500,000.

Charles amesema kuna watoto 50 ambapo wasichana ni 30 na wavulana ni 20 ikiwa wote wanasoma madarasa tofauti kuanzia awali hadi sekondari ambao waliletwa kwenye kituo hicho wakiwa yatima na wengine waliokuwa wakiishi kwenye mazingira magumu.

Masanja amesema changamoto iliyopo watoto hao hawana Bima za Afya hali wakiugua inakuwa changamoto kupata fedha za matibabu.

Pia aliomba wapatiwe ‘solar’ ili siku ukikatika watoto waweze kujisomea na kuongezewa jiko la gesi kwani ikiisha kuweka inakuwa hakuna fedha nakufika hatua ya watoto kulala njaa.

“Tunashukuru kwa msaada mkubwa mlioutoa tunaomba mkienda huko mtuangalie suala la mahitaji mengine ikiwemo vyombo vya kupikia kama sufuria zimekuwa za siku nyingi ni chakavu,” alisema Charles.

Meneja wa TRA, Wisaka Kamwamu, amesema wameamua kutoa msaada wa vitu hivyo na fedha kwa kusherekea miaka 30 ya tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo nchini ambapo hawataishia hapo wamesikia changamoto zilizopo nakwenda kuanzisha harambee ili kuweza kuzitatua.

“Kama suala la bima ya afya na gesi ya kupikia hilo suala tumelichukua nakulifanyia kazi najua kwa mapenzi ya mungu hamtaweza kulala njaa na hakuna budi sisi kama watumishi kuhudhuria kwenye kituo hiki mara kwa mara ” amesema Kamwamu.

Kaimu Meneja Msaidizi Mkoa upande wa ukaguzi TRA Kahama. Ester Martin amesema watoto hawa ni upande wa jamii wakikua ni walipa kodi wazuri hivyo wamekuja kuwaona na wapo waelewa na kipindi hiki wako karibu na walipa kodi nakushirikiana nao ili wafahamu takwa la kisheria na ulipaji kihiari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *