TANGA: Mkoa wa Tanga umepiga hatua kubwa katika utekelezaji wa mradi mkubwa wa kimkakati wa kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari wilayani Pangani, baada ya Mkuu wa Mkoa, Dk. Batilda Buriani, kuzindua rasmi mchakato wa malipo ya fidia kwa wananchi.

Mradi huo wenye Dola za Marekani milioni 350 sawa na Sh bilioni 900 unatazamwa kama mkombozi wa kiuchumi kwa mkoa huo na taifa kwa ujumla, ukitarajiwa kutoa ajira na kuimarisha sekta ya viwanda.

Katika zoezi ambapo  jumla ya wakazi 474 kutoka vijiji vya Mseko na Kigurusimba, vilivyopo Kata ya Masaika, wameanza kulipwa fidia zao ili kupisha eneo la ekari 22,000 zilizotengwa kwa ajili ya mradi huo.

Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Uwekezaji Tanzania (EPZA/TIZEZA) imesimamia ukamilishaji wa tathmini ya maeneo na mali za wananchi hao, huku maelekezo yakitolewa kuwa malipo hayo yakamilike kabla ya Juni 30, 2026.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Uwekezaji Tanzania (EPZA/TIZEZA), Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Mamlaka hiyo, Remigius  Ruttasitara, amethibitisha kuwa wanufaika 474 wataanza kupokea malipo ya fidia zao kabla ya Juni 30, 2026.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *