• Rais William Ruto ameongeza makali ya mzozo wake na Gideon Moi kuhusu madeni ambayo hayajalipwa na uadilifu wa vyombo vya habari, siku moja tu baada ya kumshutumu kwa kumhujumu kwa njia ya usaliti na vitisho
  • Rais alimtuhumu Moi kujificha nyuma ya madai ya madeni huku akidaiwa kupuuza malipo ya wafanyakazi wake
  • Kauli za Ruto zinakuja wakati akikabiliwa na ukosoaji mkali kufuatia chapisho lake la X la Jumatano ambalo lilizua maoni mseto mtandaoni

Rais William Ruto amemshambulia tena Gideon Moi huku mzozo wao ukiendelea kushika kasi kwenye mtandao wa X.

Rais William Ruto na Gideon Moi
Rais William Ruto na Gideon Moi wakiwa Ikulu. Picha: William Ruto
Source: Facebook

Rais William Ruto ameongeza mashambulizi yake dhidi ya Gideon Moi kuhusu madeni ambayo hayajalipwa na uadilifu wa vyombo vya habari, siku moja tu baada ya kumshutumu kwa madai ya kumhujumu kwa njia ya usaliti na vitisho vya habari.

Rais alimtuhumu Moi kujificha nyuma ya madai ya madeni huku akidaiwa kupuuza malipo ya wafanyakazi wake.

Kauli za Ruto zinakuja wakati akikabiliwa na ukosoaji mkali kufuatia chapisho lake la X la Jumatano ambalo lilizua hisia mseto mtandaoni.

Pia soma

Ruto afichua kilichovunja maridhiano yake na Gideon Moi baada ya miezi minane ya usuhuba

Rais William Ruto amemshambulia tena Gideon Moi huku mzozo wao ukiendelea kushika kasi kwenye X.

Katika chapisho jingine mapema Alhamisi asubuhi, Juni 25, rais alijibu madai ya gazeti la The Standard kwamba serikali inaidaiwa KSh 1.2 bilioni za malipo ambayo hayajalipwa.

Katika chapisho ambalo lilifanana kwa kiasi kikubwa na lile la Jumatano kwa mtindo wa uandishi na sarufi, Rais Ruto alimtuhumu mwenyekiti wa KANU kujificha nyuma ya madai hayo ya deni ili kuepuka kuwalipa wafanyakazi wake kwa miezi mingi.

Pia alimtuhumu Moi kwa kudhoofisha uadilifu wa taaluma ya uandishi wa habari ambao The Standard iliwahi kujivunia kupitia vichwa vya habari vya kushtua vinavyolenga serikali yake.

“Bro, wewe bilionea ulivyo; kujificha nyuma ya ‘madeni’; kuwafanya wafanyakazi wafanye kazi kwa miezi mingi bila malipo wakitetea uhalifu wa vichwa vya habari vya The Standard vinavyoendeshwa kwa tamaa na ulaghai; ni ukatili kwa wafanyakazi waaminifu, ni dharau kwa uandishi wa habari na ni usaliti kwa vyombo huru vya habari ambavyo The Standard iliwahi kuwakilisha,” Ruto aliandika kwenye X.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya rais kutumia X kumshambulia Moi, ambaye familia yake inahusishwa na umiliki wa kampuni ya habari ya The Standard yenye makao yake kwenye Barabara ya Mombasa.

Pia soma

“Hata Rais Husoma Standard”: Gazeti Lamjibu Ruto kwa Mkwara wa Kejeli

Rais alikuwa amemtuhumu Moi kwa kutumia vichwa vya habari vya kushtua kumshinikiza na kumhujumu kisiasa.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *