
Maseneta nchini Nigeria, wamepitisha mswada, utakaoruhusu majimbo nchini humo kuwa na vikosi vyao vya polisi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hatua hii inakuja baada ya bunge la kitaifa kupitisha mswada huo mapema mwezi huu, ambao unalenga kubadilisha sekta ya usalama nchini Nigeria.
Hii inakuja wakati huu serikali ya Nigeria, ikiendelea kukabiliwa na changamoto kubwa ya kukabiliana na utovu wa usalama, katika majimbo yote 36.
Baada ya hatua hiyo, wawakilishi kutoka majimbo yote wanatarajiwa kupitisha mswada huo, kabla ya kuanza kutekelezwa.
Rais Bola Tinubu, anaunga mkono mabadiliko hayo, anayosema kila jimbo kuwa na kikosi chake cha polisi, itasaidia kuimarisha usalama nchini humo.
Wanaounga mkono mabadiliko hayo wanasema pia hatua hiyo itatoa fursa kwa uundaji kwa kikosi cha polisi kinachoelewa jimbo husika, na itakuwa rahisi kuwaajibisha katika majukumu yao.