Mfumo “wa kina” wa uhakiki unahitajika nchini Iran baada ya mzozo wa hivi majuzi ili kuhakikisha nchi hiyo haitengenezi silaha za nyuklia, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) amesema leo Ijumaa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Nadhani lengo la makubaliano haya (ya hivi majuzi kati ya Marekani na Iran) ni kuhakikisha kwamba hakuna maendeleo ya silaha za nyuklia nchini Iran. Serikali ya Iran imesema kwa uwazi kabisa kwamba hii sio nia yake,” Rafael Grossi amesema katika mkutano na waandishi wa habari huko Japan.

“Lakini bila shaka, nia haitoshi. Tunahitaji kuweka mfumo wa uhakiki wa kina (…) haraka iwezekanavyo,” ameongeza Rafael Grossi.

Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki unatarajia kukagua maeneo ya nyuklia ya Iran ‘haraka iwezekanavyo’

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki la Umoja wa Mataifa (IAEA) Rafael Grossi amesema shirika hilo limepewa jukumu la kukagua maeneo ya nyuklia ya Iran kama sehemu ya makubaliano ya Marekani na Iran.

“Mkataba huu wa maelewano unabainisha wazi kwamba kipengele cha nyuklia cha mkataba huo kitasimamiwa […] na IAEA. Ili kuhakikisha usimamizi huu tunapaswa kufanya ukaguzi, hakuna njia nyingine, Rafael Grossi amewaambia waandishi wa habari huko Tokyo, Japan. Kazi ya kiufundi imeanza na tunatarajia kuwa katika maeneo husika hivi karibuni.”

Rafael Grossi ameongeza: “IAEA lazima iwe na ufikiaji wa maeneo na kuyakagua. Niko tayari kuendelea na kazi ya kiufundi na kufika kwenye maeneo husika haraka iwezekanavyo. “

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *