Jumuiya ya kimataifa imeendelea kutuma misaada ya kibinadamu na wataalamu wa uokoaji nchini Venezuela, wakati huu vikosi vya uokoaji kwenye nchi hiyo vikiendelea na utafutaji wa watu wanaodhaniwa kufukiwa kwenye vifusi vya jengo yaliyoanguka kutokana na tetemeko la ardhi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na rais wa kipindi cha mpito nchini humo, Delcy Rodriguez, umoja wa Mataifa umetuma wataalamu wake wa masuala ya majanga kwenda kuongeza nguvu za uokoaji na utafutaji.

Aidha mataifa ya Ulaya kama vile Uswis na Uholanzi zilitangaza kutuma wafanyakazi wake wa uokoaji zaidi ya 80 pamoja na tani 18 za misaada mingine.

Maofisa kutoka idara ya wazima moto nchini Chile ikiwasili nchini Venezuela.
Maofisa kutoka idara ya wazima moto nchini Chile ikiwasili nchini Venezuela. REUTERS – Pablo Sanhueza

Nchi ya Marekani kwa upande wake imetangaza kuwa inakusanya kiasi cha dola milioni 150 na kwamba imetuma meli mbili kubwa za kivita pamoja na ndege za uokoaji kwenda kusaidia juhudi za uokoaji.

Kadhalika China na mataifa ya America kusini nayo yametangaza kusimama pamoja na Venezuela, ambapo nazo zimetuma wataalamu wake wa uokoaji wakiwemo mbwa.

Shughuli ya uokoaji ikiendelea nchini Venezuela baada ya tetemeko la ardhi.
Shughuli ya uokoaji ikiendelea nchini Venezuela baada ya tetemeko la ardhi. REUTERS – Leonardo Fernandez Viloria

Mpaka sasa watu zaidi ya 230 wameripotiwa kufa na wengine elfu 1 na 500 wamejeruhiwa kufuatia tetemeko la ardhi lililokuwa na ukubwa wa 7.5 kwenye kipimo cha Richa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *