Waokoaji wa kimataifa wamewasili nchini Venezuela ambako wanaendelea na shughuli ya kuwatafuta manusura wa matetemeko mawili ya ardhi, yaliyotokea siku ya Jumatano, huku idadi ya vifo ikiongezeka na kufikia 235.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mpaka kufikia siku uya Ijumaa, watu ambao hawajaonekana, wanaaminiwa kukwama kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka baada ya matetemeko hayo ya ardhi.
Watalaam kutoka Umoja wa Mataifa na nchi kama Brazil, Mexico na Marekani wametuma watalaam wao kusaidia kuwatafuta manusura, huku yakituma pia misaada ya kibinadamu kwa manusura.
Tom Fletcher, Mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia misaada ya kibinadamu, amewaambia raia wa Venezuela kuwa, watalaam hao wanafanya kila kinachowezekana ili kuwapata wapendwa wao hawajaonekana.
Mbali na mauaji ya watu, wengine zaidi ya 4,300, wamejeruhiwa na hospitalini nyingi jijini Caracas zimejaa majeruhi.
Waziri Mkuu Diosdado Cabello, amesema matetemeko hayo ya ardhi yamesababisha nchi hiyo kupoteza kila kitu, huku eneo La Guaira, Kaskazini mwa Caracas, likiathiriwa zaidi.