Nchini Uganda, vikosi vya usalama vimevamia makaazi ya wanasiasa wawili mashuhuri  wanawake, ambao wamekuwa katika mstari wa mbele kutetea haki za binadamu na kuukosoa utawala wa rais Yoweri Museveni.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Uvamizi huo ulilenga nyumba ya Dkt. Miria Matembe ambaye pia ni waziri wa zamani na mbunge na Dkt Sarah Bireete anayeongoza shirika linayotetea uzingatiaji wa katiba na utawala bora.

Dkt. Matembe hakuwepo nyumbani kwake wakati kitendo hiki kilitokea na tangu wakati huo hajaonekana wala kusikika. Dkt Sarah Bireete anasimulia kilichotokea nyumbani kwake.

Sarah Bireete, kiongozi wa shirika linayotetea uzingatiaji wa katiba na utawala bora

“Nyumba yangu ilivamiwa na askari wapatao 20, walipindua kila kitu, walivunja milango na kuiba pesa. Wanatumia nguvu za serikali kuwanyanyasa wanawake. Ni aibu kubwa kwa rais Museveni na ninamwomba azungumzie kuzorota kwa utawala wa sheria kwenye nchi hii.” Amesema Sarah Bireete.

Lakini kitendo hiki kinamaanisha nini kwa Uganda? Mwanaharakati Penelope Sanyu anaeleza.

“Uvamizi wa nyumba, unyanyasaji wa raia na wanaharakati sio dalili za demokrasia bali ni mbinu za ukandamizaji. Munachofanya ni makosa na munavunja misingi vya demokrasia.”  Ameeleza Mwanaharakati Penelope Sanyu anaeleza.

Winnie Kiiza, kiongozi wa zamani wa upinzani katika bunge la Uganda naye amekuwa na kauli hii.

“Watu wanakamatwa na kushambuliwa lakini mtu ambaye anajitoa kama kiongozi kuzungumzia hili, tunampa ujumbe Rais, anastahili kuwadhibiti wanajeshi wake kuanzia kwa kijana wake.” Amesema Winnie Kiiza.

Hali hii ilijitokeza siku chache baada ya wanaharakati hao wanawake kumkosoa kamanda wa jeshi ambaye pia ni mtoto wa rais Museveni Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuhusu namna Wakili Erias Lukwago alivyokamatwa.

Kenneth Lukwago, Kampala RFI, Kiswahili 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *