
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3
Ukosefu wa imani na kuaminiana katika uhusiano, ambao unaweza kufanya kuishi pamoja kuwa na migogoro au wasiwasi, na hatimaye unaweza kusababisha kutengana.
Ni hali ambapo mmoja au wote wawili katika uhusiano hawaaminiani kikamilifu au hawawezi kutegemeana.
Kwa mfano, mume hakubali mke wake anapokwenda nje, au mke hakubali mume wake. Vivyo hivyo, kati ya kijana na msichana, msichana anamshutumu mpenzi wake kwa kutokuwa mwaminifu au kijana anamshutumu msichana wake.
Swali hapa ni ni nini husababisha ukosefu huo wa imani ambao unaweza kusababisha talaka au kutengana kwa wenza wanaoishi pamoja.
BBC ilizungumza na Maryam Hassan Baba, mtaalamu wa masuala ya familia na mmiliki wa ukurasa wa Instagram unaoitwa The Northern Therapist.
Sababu za kutoridhika
Mtaalamu huyo alitaja sababu tano kuu zinazochochea ukosefu wa imani kati ya wapenzi:
1. Ukosefu wa mawasiliano bora:
Mara nyingi, wanandoa au wapenzi hukosa njia sahihi ya kuwasiliana, hasa wanapokumbana na tofauti au migogoro. Ukweli unapofichwa au hisia kama hasira na wasiwasi hazizungumzwi wazi, hujenga pengo la kutoelewana na hatimaye kutokuaminiana.
2. Kuvunja ahadi:
Kuvunja ahadi, usaliti, au kuchepuka huharibu kabisa msingi wa uaminifu kati ya wapenzi.
3. Uongo wa mara kwa mara:
Uongo wa mara kwa mara, hasa kuficha mambo muhimu kutoka kwa mwenzi, hujenga mashaka na hatimaye husababisha kutokuaminiana.
4. Wivu na mashaka kupita kiasi:
Wivu uliopitiliza husababisha hofu ya kumpoteza mwenzi, na huweza kuleta tuhuma zisizo na msingi ambazo huharibu uhusiano.
5. Kukosa heshima:
Kudharau, kutukana, au kupuuza maoni ya mwenzi huondoa heshima ya pande zote na kupunguza kabisa imani katika uhusiano.
Kwa ujumla, sababu hizi zote huanza kidogo lakini zikiruhusiwa kuendelea, huweza kuharibu kabisa msingi wa uhusiano.
Njia za kurekebisha changamoto katika mahusiano
Chanzo cha picha, Getty Images
Maryam Hassan Baba, mtaalamu wa masuala ya familia na mmiliki wa ukurasa wa Instagram Maryam Hassan Baba wa The Northern Therapist, pia alieleza njia nne za kurekebisha mahusiano yanapokuwa yameingia matatani:
Kuzungumza kwa utulivu na kwa uaminifu:
Ni muhimu wenza kuzungumza bila hasira, kwa uwazi na kwa nia ya kuelewana.
Kujenga imani kupitia uaminifu na kutimiza ahadi:
Kuwa mkweli na kuhakikisha ahadi zinazotolewa zinatekelezwa husaidia kurejesha imani.
Kuheshimiana wakati wote:
Kuheshimu hisia, maoni na utu wa mwenzi ni msingi muhimu wa kurekebisha uhusiano.
Kutafuta ushauri pale tatizo linapokuwa kubwa:
Wakati changamoto ni nzito, msaada wa mtaalamu au mshauri wa mahusiano unaweza kusaidia sana.
Mambo 6 ambayo wenza hawapaswi kamwe kuambiana
Watu wengi hutumia aina fulani ya mawasiliano kuwaonyesha wenzi wao kwamba wana tatizo la akili. Hata hivyo, mara nyingi hufanya hivi kwa sababu wanatafuta kitu ndani ya mtu mwingine.
Mtaalamu aliorodhesha njia 6 kama ifuatavyo:
- Wazimu / Mwendawazimu
- “Natania.”
- Wewe ndiye uliyenisababisha kufanya hivi , Ni kosa lako
- Ikiwa unataka, unaweza kufanya hivyo, niache tu peke yangu.
- Kila mtu anakubaliana nami isipokuwa wewe.
- Wewe ndiye tatizo kubwa zaidi.