• Madaktari mara nyingi huwa hawaelewi nini sababu ya baadhi ya wanawake kupatwa na maumivu hayo ilhali wengine huhisi tu kawaida wakati wa hedhi
  • Hata hivyo katika kutafuta suluhu ya maumivu ya wakati wa hedhi, wataalamu hasa madaktari wanashauri kutumia mbinu rahisi zisizoleta au kuongeza maumivu hayo

Ni wakati mwingine wa mwezi ambapo unapata maumivu makali kwa sababu ya hedhi. Unahisi mgonjwa kwa siku tatu au hata zaidi kutokana na hilo.

Njia 15 Rahisi Zinazosemekana Kuwa Bora Katika Kupunguza Makali ya Maumivu Yanayotokana na Hedhi
Wakati wa hedhi wengi wa wanawake hupatwa na maumivu makali lakini baadhi ya wanawake hupata maumivu kiasi tu. Picha: Her World
Source: UGC

Madaktari mara nyingi huwa hawaelewi nini sababu ya baadhi ya wanawake kupatwa na maumivu hayo huku wengine wakijihisi kawaida wakati wa hedhi.

Lakini huenda kuna sababu kadha ambazo zinaweza kuhusishwa na maumivu haya na ni pamoja na uvimbe katika nyungu ya uzazi na matumizi ya dawa za kuzuia upatikanaji wa mimba.

Hata hivyo katika kutafuta suluhu ya maumivu ya wakati wa hedhi, wataalamu hasa madaktari wanashauri kutumia mbinu rahisi zisizoleta au kuongeza maumivu hayo.

Zifuatazo ni njia zinazoweza kukusaidia kukabiliana na hali hiyo.

Pia soma

Je, Sukuma Wiki Yako ni Salama? Unachopaswa Kujua Ukiwa Mnunuzi Nairobi

1. Kunywa maji kwa wingi

2. Jikande tumboni kwa kitambaa chenye joto labda ulichotumbukiza kwenye maji ya moto kiasi

3. Epuka vyakula vinavyofurisha tumbo mfano vyakula vyenye mafuta mengi

4. Tumia miti shamba kama vile aina ya majani chai

5. Kunywa chai kabla ya hedhi kuanza

6. Tumia mafuta ya samaki au vitamin B1.

7. Kula chakula bora-epuka vyakula vilivyo laini sana, vyenye nyuzi au maharagwe

8. Tumia madini kama vile magnesium

9. Ondoa shinikizo la damu kwa kudunga maeneo maalum mwilini (acuapuncture)

10. Fanya ngono salama

11. Tumia dawa za kutuliza maumivu

12. Tumia vikinga mimba

13. Pata usingizi wa kutosha

14. Fanya mazoezi

15. Jikande kwa kutumia mafuta maalum

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *