Baada ya siku kadhaa za mashambulizi ya pande zote ambayo karibu yavunje makubaliano ya kusitisha mapigano, Washington na Tehran zimekubaliana kusitsha mashambulizi yao na kuanza tena mazungumzo  siku ya Jumanne nchini Qatar.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Iran na Marekani zimekubaliana kukomesha mashambulizi ya hivi karibuni katika Ghuba na kuanza tena mazungumzo kuhusu mzozo wao kuhusu Mlango-Bahari wa Hormuz, afisa wa Marekani alisema siku ya Jumapili, Juni 28, na kuzua matumaini ya kuokoa makubaliano ya amani yaliyodhoofishwa na mashambulizi ya pande zote ya siku kadhaa. “Majadiliano ya kiufundi yanapaswa kuendelea katika poiti zote ya itifaki ya makubaliano. Pande zote mbili zinasitisha mashambulizi yao kwa sasa, na meli zinaweza kusafiri kwa uhuru,” afisa huyo alisema, akimaanisha itifaki ya makubaliano ya pointi 14 yaliyofikiwa Juni 17, ambapo mlango-bahari huo ungefunguliwa tena kwa ajili ya usafiri.

Axios, chombo cha kwanza cha habari kuripoti kusitishwa kwa uhasama, kikimnukuu afisa mkuu wa Marekani, kilibainisha kuwa mazungumzo yataanza tena Jumanne nchini Qatar.

Kurudi huku kwa diplomasia kunakuja baada ya siku kadhaa za mashambulizi na majibu tangu kombora la Iran lilipogonga meli ya mizigo katika Mlango-Bahari wa Hormuz siku ya Alhamisi, huku Marekani na Iran zikishutumiana kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa Juni 17. Iran ilirusha makombora na ndege zisizo na rubani katika maeneo ya kijeshi ya Marekani huko Kuwait na Bahrain mapema siku ya Jumapili asubuhi, muda mfupi baada ya Rais Donald Trump kutishia “kuiangamiza” Jamhuri ya Kiislamu ikiwa haitafuata makubaliano ya kukomesha vita.

Wakati huo huo, Israel ilitangaza Jumapili kwamba imefanya shambulio lingine dhidi ya Hezbollah, kundi lenye silaha linaloungwa mkono na Iran, nchini Lebanon. Shambulio hilo liliharibu miundombinu ya chini ya ardhi inayotumiwa na wapiganaji wa Kiislamu katika kijiji kusini mwa Lebanon. Shambulio hili linafuatia shambulio la awali siku ya Jumamosi, muda mfupi baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa na Lebanon siku ya Ijumaa. Iran inasisitiza kwamba mapigano nchini Lebanon lazima yasitishwe ili makubaliano yote yaheshimiwe. Jeshi la Marekani lilisema mapema kwamba lilishambulia Iran tena, saa chache baada ya meli ya mafuta kushambuliwa katika Mlango-Bahari wa Hormuz, njia muhimu zaidi ya majini duniani kwa ajili ya usafiri wa nishati, ambayo Tehran imeifunga kwa kiasi kikubwa kwa muda mwingi wa mzozo.

“Huenda ikafika wakati ambapo hatutaweza tena kutenda kwa busara na kulazimishwa kukamilisha, kwa nguvu za kijeshi, kazi tuliyoianza vizuri sana,” Donald Trump alitangaza kwenye mitandao ya kijamii kabla ya makala ya Axios kuchapishwa. “Ikiwa hilo litatokea, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitakuepo!” aliongeza.

Makubaliano dhaifu ya usitishaji mapigano 

Duru ya kwanza ya mazungumzo, yaliyoongozwa na Makamu wa Rais J.D. Vance na Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, yalifanyika Uswisi wiki moja iliyopita, na Washington iliondoa vikwazo dhidi ya Tehran, lakini mapigano yameanza tena na yameongezeka.

Karibu saa moja baada ya ujumbe wa Donald Trump kuchapishwa, jeshi la Kuwait liliripoti kwamba ulinzi wake wa anga ulijibu mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani, huku Bahrain ikibainidha kwamba ving’ora vililia ndani ya mipaka yake. Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu cha Iran kilisema katika taarifa kwamba jeshi lake la wanamaji na anga limeanzisha operesheni za makombora na ndege zisizo na rubani kulenga maeneo ya kijeshi ya Marekani huko Kuwait na Bahrain.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *