
Nchini Uganda, kundi kuu la vyombo vya habari huru nchini humo linadai kuzingirwa na jeshi. NTV, Daily Monitor, na vituo vingine kadhaa vya redio viliacha kutangaza usiku wa kuanzia Jumamosi, Juni 27, kuamkia Jumapili, Juni 28, kwa amri ya Jenerali Muhoozi Kainerugaba, mkuu wa majeshi ya Uganda na mtoto wa Rais Yoweri Museveni. Wanajeshi wanapiga kambi nje ya ofisi zao jijini Kampala. Jenerali huyo alitangaza nia yake mpya siku ya Jumapili kupitia mtandao wa kijamii wa X.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“NTV na Monitor zimefungwa hadi leo,” Jenerali Muhoozi Kainerugaba alitangaza usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili.
Mkuu wa jeshi anadai “kutoamini katika uhuru wa vyombo vya habari” na anabainisha kuwa baba yake, Rais Yoweri Museveni, aliidhinisha operesheni hiyo.
Ofisi “zimezingirwa na jeshi”
Katika machapisho yao kwenye mitandao ya kijamii, vyombo hivyo viwili vya habari vilibainisha kwamba “vimezingirwa na jeshi,” huku askari wakipiga kambi nje ya ofisi zao katika mji mkuu, Kampala.
“Tumefungwa na jeshi, katika studio na ofisi za NTV,” mwandishi wa habari mkongwe kutoka kituo hicho aliliambia shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa jina. “Hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia au kutoka. Wale waliokuwa wakifanya kazi jana usiku waliamriwa na jeshi kuondoka.”
“NTV Uganda na Spark TV zililazimishwa kusitisha matangazo yao huku Daily Monitor ikifungwa kwa amri ya Jenerali Muhoozi,” gazeti hilo pia liliandika kwenye mitandao ya kijamii.
Vituo hivyo viliacha kutangaza mapema siku ya Jumapili. “Video haipatikani,” ulisomeka ujumbe huu kwenye vituo vyao vya kawaida vya utangazaji, kulingana na vyombo vya habari vya ndani. Vyombo vingine vya habari katika kundi hilo, ikiwa ni pamoja na Dembe FM, KFM, na The East African, pia viliathiriwa.
Huu ni “mwanzo tu, tutawakamata watu wengi zaidi”
Shambulio hili linakuja pamoja na miezi kadhaa ya kukamatwa kwa wanasiasa na wanaharakati, hatua iliyochukuliwa na mkuu wa jeshi la Uganda. Kwa waangalizi wengi wanasema, hivyo anaandaa urithi wake kama mkuu wa nchi.
Hii si mara ya kwanza Daily Monitor kulengwa. Gazeti hilo tayari lililazimishwa kusitisha mata kufanya shughuli zake kwa siku 13 mwaka 2013, baada ya kuripoti kuhusu njama inayodaiwa ya kumtaka Muhoozi Kainerugaba kumrithi baba yake.
Siku ya Jumapili, kwenye mitandao ya kijamii, jenerali huyo aliendelea zaidi, akiongeza kwamba “kufungwa kwa NTV na Monitor ni mwanzo tu; tutawakamata watu wengi zaidi.”
Kipindi cha Afrika cha Kamati ya Kuwalinda Waandishi wa Habari (CPJ) kililaani ongezeko hili la kutisha. Uganda inashika nafasi ya 143 kati ya nchi 180 katika Orodha ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ya Shirika la Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka (RSF).