#HABARI: Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amewaahidi vinyozi na wasusi kuwa anakwenda kumuomba Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili awape mikopo.
Makonda amesema hayo jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa Chama cha Wasusi na Vinyozi (Chama cha Saloonist Tanzania) chenye lengo la kurasimisha sekta hiyo, kulinda haki za wafanyakazi, na kutengeneza mazingira salama ya kupata mikopo, vifaa vya kisasa, pamoja na mafunzo ya kitaluma yatakayosaidia kukuza vipaji vya vijana wajasiriamali ambapo Mlezi wa Chama hicho ni Jokate Mwegelo (Jokate Urban Mwegelo) kupitia Kidoti Foundation.
Makonda amesema “Mnaofanya kazi saluni nawasihi achaneni na ushirikina mkaribisheni Mungu kwenye saluni zenu ili muone mkono wake, jambo la pili nawaomba sana wenye saluni na Wafanyakazi muwe sehemu ya kulinda amani ya Taifa letu, hakuna Mtu atakuja kunyoa au kusuka kama hakuna amani, wala hatuoona harusi au Mtu amekaa anasuguliwa miguu kama kuna vita, hakikisheni saluni zote nchini zinahubiri amani”
Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITV EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
Follow ITV TANZANIA RadioOne Tanzania
Capitalradio Tanzania
(Feed generated with FetchRSS)