Benki ya NMB imeendelea kudhihirisha mchango wake katika uchumi wa Taifa baada ya kutunukiwa tuzo ya kuwa miongoni mwa walipa kodi wakubwa nchini.
Tuzo hiyo imetolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika hafla ya Tuzo za Rais kwa Walipakodi Bora iliyofanyika sambamba na maadhimisho ya miaka 30 ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Tuzo hiyo imepokewa na Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna.
Hafla hiyo pia imetumika kutambua walipakodi walioonyesha uzalendo na uwajibikaji, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 ya TRA tangu kuanzishwa kwake.
Mhariri | @rajjmsangi
#AzamTvUpdates
(Feed generated with FetchRSS)