
Nchini Mali, mashambulizi yaliyoratibiwa yamefanyika Jumamosi katika angalau maeneo sita kaskazini, katikati, na kusini mwa nchi. Serikali inabainisha kwamba hali iko chini ya udhibiti. Muungano wa makundi ya wanajihadi yenye uhusiano na Al Qaeda na waasi wanaoataka kujitenga wa Azawad Liberation Front (FLA) unadai kuwa umefikia malengo yake.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu wa kikanda, Serge Daniel
Makabiliano makubwa yalifanyika katika mji wa Anéfis kaskazini mwa Mali. Baada ya mapigano ya saa mbili, waasi wanaotaka kujitenga wa FLN (Forces Laïques d’Algérie) wanashikilia eneo hili la kimkakati, wakiwashikilia mateka wanajeshi wengi wa jeshi la Mali. Mamluki wa Urusi, wanaounga mkono vikosi vya jeshi la serikali, wamekusanya tena katika kambi ya kijeshi ya mji huo, ambapo walikuwepo tangu Jumamosi usiku.
Huko Gao, jiji kuu kaskazini mwa Mali, na katika miji mitatu katikati mwa nchi, muungano wa makundi ya waasi unawashikilia wanajeshi wa seikali. Jeshi la Mali, kwa upande wake, linadai kurudisha nyuma shambulio hilo na kusababisha hasara kubwa kwa adui. Kusini zaidi, kilomita chache kutoka mji mkuu wa Mali, wanajihadi waliohusishwa na Al Qaeda walizindua shambulio kubwa kwenye gereza la raia kabla ya kuondoka.
Miji ya Bamako na, haswa, Kati, ngome ya utawala wa kijeshi haikukumbwa na mashambulizi haya yaliyoratibiwa. Kwa waangalizi, huu ni uthibitisho kwamba mashambulizi yanaweza kuendelea.