
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, utafutaji unaendelea baada ya boti moja kuzama katika makutano ya mito ya Kasai na Sankuru katika eneo la Ilebo. Idadi ya muda vifo iliyotolewa na mamlaka siku ya Ijumaa, Julai 3, inafikia angalau 20, huku manusura 80 na zaidi ya watu 100 wakiwa bado hawajapatikana. Utafutaji unaendelea kwa kutumia mitumbwi yenye injini ili kujaribu kuwapata wengi waliotoweka. Kulingana na afisa wa shirika la Msalaba Mwekundu katika eneo hilo, matumaini ni madogo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu mjini Kinshasa, Pascal Mulegwa
Juhudi za uokoaji zimekuwa zikiendelea kwenye kingo za mto siku ya Jumamosi alasiri, Julai 4, kutafuta manusura au miili ya watu waliotoweka.
Kulingana na François Kabula, mkuu wa eneo la Ilebo, zaidi ya watu 200 walikuwa ndani ya boti hiyo, iliyokuwa ikisafiri kutoka bandari ya Kalina kwenda Ilebo, katika eneo la Sankuru. Miongoni mwa abiria walikuwa wanafunzi wengi wakirudi nyumbani baada ya mitihani yao ya serikali.
Kulingana na vyanzo kadhaa vya ndani na vyanzo rasmi, boti iliondoka bandarini usiku ili kukwepa ukaguzi wa usalama, licha ya kuwa imejaa abiria na mizigo mingi.
Watu 80 waliokolewa
Katika makutano ya mito ya Kasai na Sankuru, mtumbwi huo ulivunjika kabla ya kuzama. Watu themanini waliokolewa kutokana na uingiliaji kati wa wavuvi walio kuwa karibu.
Ajali hii ni miongoni mwa ajali mbaya zaidi tangu mwanzo wa mwaka. Wengi wameshtumu mazingira ya usafiri.
Asasi za kiraia huko Ilebo zinalaani kutafuta faida kwa gharama ya usalama wa abiria na kudai vikwazo dhidi ya wamiliki wa meli, udhibiti mkali hata usiku, na jaketi za lazima za kuokoa maisha.
Takwimu zinazoshikiliwa na mamlaka ya uhamiaji ni za chini sana kuliko idadi halisi ya watu waliokuwemo ndani ya boti. Mamlaka ya uhamiaji inawezaje kutoa taarifa ya abiria 30 wakati tayari kuna manusura 80″ , amesma Pierre Sosthène Kambidi (mbunge wa mkoa huko Kasai Central), na kuongeza “boti ilikuwa ya zamani na ilikuwa imejaa watu.”