Ujumbe kutoka Algeria ambao ni sehemu ya kamati ya ngazi ya juu ya amani na usalama ya Umoja wa Afrika umewasili nchini Sudan Kusini kutathmini hatua zilizopigiwa katika mpango wa utekelezwaji wa mkataba wa amani.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wajumbe hao wanatarajiwa kukutana na maofisa wa serikali ya Juba na washirika wengine muhimu kuangazia hatua zilizopigiwa kuelekea utekelezwaji wa mchakato wa amani.

Aidha wanatarajiwa kutathmini maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Disemba 22 mwaka huu, huku wajumbe wengine wamepangiwa kuwasili Juba Jumatatu ya leo.

Kamati ya amani na usalama katika Umoja wa Afrika kwa sasa ipo chini ya Uenyekiti wa Afrika Kusini, nchi za Chad, Nigeria, Algeria na Rwanda zikiwa na wawakilsihi kwenye kamati hiyo.

Wajumbe hao watakuwa Sudan Kusini kwa kipindi cha siku mbili, kuanzia leo Jumatatu hao kesho Jumanne.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *