Mfanyabiashara mashuhuri nchini na Mwenyekiti wa Kampuni za Bakhresa, Saidi Salim Bakhresa, ametunukiwa Tuzo ya ‘Pioneer of Made in Tanzania’ kwa kutambua mchango wake wa kuwa miongoni mwa waanzilishi na vinara wa kukuza bidhaa zinazozalishwa nchini.

Tuzo hiyo imekabidhiwa na Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ikiwa ni heshima kwa mchango wake mkubwa katika kukuza viwanda na uzalishaji wa bidhaa za ndani.

Mhariri | @rajjmsangi
#AzamTvUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *