Mfanyabiashara mashuhuri nchini, Saidi Salim Bakhresa, ametunukiwa Tuzo ya Kinara wa Sekta ya Viwanda ( Industrial Champion Award ) ikiwa ni kutambua mchango wake mkubwa katika maendeleo ya sekta ya viwanda, biashara na uchumi wa Tanzania.
Tuzo hiyo imekabidhiwa na Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi, katika hafla ya Tuzo za Dhahabu na Maadhimisho ya Saba saba iliyofanyika Mlimani City, Dar es Salaam.
Kutunukiwa kwa Bakhresa kunadhihirisha kutambuliwa kwa mchango wake wa muda mrefu katika kukuza viwanda, kuzalisha ajira na kuchochea maendeleo ya uchumi wa taifa.
Mhariri | @rajjmsangi
#AzamTvUpdates
(Feed generated with FetchRSS)