Uhamisho wa kimatibabu kwa waliojeruhiwa nchini Sudan Kusini uliongezeka kwa asilimia 50 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2026, Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu imesema, wakati huu machafuko kwenye nchi hiyo yakipunguza upatikanaji wa huduma za afya.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Taifa hilo changa zaidi duniani, limeshuhudia miezi kadhaa ya machafuko mapya tangu mwaka 2025, ambapo vikosi tiifu vya rais Salva Kiir vinapambana na wapiganaji wenye uhusiano na mpinzani wake Riek Machar, katika miji kadhaa nchini humo.
Kwa mujibu wa ICRC, imewahamisha majeruhi zaidi ya 266 kati ya mwezi Januari na Juni mwaka huu, idadi hii ikivuka asilimia 50 ya majeruhi iliyowahamisha katika kipindi hiki hiki mwaka uliopita.
Taarifa ya shirika hilo imeongeza kuwa, kiwango hiki kimechangiwa na ongezeko la mapigano ambapo raia zaidi ya Elfu 1 na 300 wameathirika, ikiwemo vifo 767, hili likiwa ni ongezeko la asilimia 89.
Sudan Kusini ilipata uhuru mwaka 2011, lakini punde tu taifa hilo lilitumbukia katika vita ya wenyewe kwa wenyewe kati ya vikosi vya rais Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake wa kwanza wa rais, Riek Machar, vita ambayo ilipelekea kupatikana kwa mkataba wa amani wa mwaka 2018.