Wawakilishi wa upinzani wa DR Congo, walioalikwa Bujumbura kwa mashauriano na Rais wa  Burundi ambaye pia ni mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika AU, wamependekeza rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo kama mpatanishi.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Jukumu lake ni kutatua mgogoro wa kisiasa, kitaasisi, na usalama unaozua hofu ya kutokea kwa machafuko mkubwa.

Julai 6, Rais Evariste Ndayishimiye alizileta pamoja pande mbalimbali, kwenye mashauriano, yaliyofanyika katika Ikulu ya Ntare kati ya wawakilishi wa upinzani wa DR Congo na wawakilishi wa madhehebu ya kidini, wakiwemo viongozi wa makanisa ya Pentekoste, wajumbe kutoka ECC (Kanisa la Kikkristo nchini Kongo), na CENCO (Baraza la Kitaifa wa Maaskofu wa Kongo), tayari wameonyesha ukomo wa kile ambacho hakitakiwi kufikiwa, ambacho wanakiita “mstari mwekundu” ambao haupaswi kuvukwa. Wameweka mambo matatu muhimu.

Kwanza kabisa wanapendekeza kuwepo na upatanishi. C64, Muungano wa Upinzani wa Kutetea Katiba, ambao unachukua jina lake kutoka Kifungu cha 64 cha Sheria ya Msingi, inayowaamuru kila raia kupinga kunyang’anywa au kutumia mamlaka yoyote kinyume na maandishi haya matakatifu, tayari imeeleza msimamo wake.

Unapendekeza upatanishi uongozwe na Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo. Yeye si mgeni katika aina hii ya kazi. Kwa ajili ya dhamira hii nzuri, wanachama hawa wa upinzani wanapendekeza kwamba CENCO na ECC ziwe sehemu muhimu ya utaratibu huu, kutokana na uaminifu wao, utaalamu, na uzoefu katika eneo hili.

Kwa muungano huu, unaowakilishwa hasa na watu kama Martin Fayulu, hoja ya pili ya mjadala ni mpango wa kurekebisha Katiba.

“Washiriki hawapaswi kuchaguliwa na Rais Tshisekedi.”

Kulingana na kundi hili, Rais Tshisekedi lazima ajitoe hadharani kuachana na mpango huu, ambao wanauelezea kama “mpango mbaya ambao unaweza kufungua njia ya muhula wa tatu wa urais, ingawa unaisha mwaka wa 2028.”

Kama sharti la tatu, wanachama hawa wa upinzani wanataka mazungumzo jumuishi na kukataa “mashauriano yaliyopangwa kulingana na matakwa na ajenda ya serikali. Washiriki hawapaswi kuwa watu waliochaguliwa na rais Tshisekedi.”

Wajumbe hawa wa upinzani wanakataa kutengwa na kudai ushiriki wa watendaji wote wa kisiasa na kijamii nchini. Hii inakuja wakati ambapo baadhi ya watendaji tayari wanaonekana kuondolewa au kutengwa.

Wingi wa vyama madarakani umekuwa wazi na kudai kuwa mashauriano na watu kama Corneille Nangaa, Bertrand Bisimwa, na Joseph Kabila, ambao wanachukuliwa kuwa ndio waliohusika na vurugu zilizofanywa Kaskazini na Kusini mwa Kivu, hayawezi kufanyika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *