Rais wa Nigeria Bola Tinubu, ameagiza uchunguzi kuhusu madai ya rushwa kubaini ripoti kuwa kitengo kisichokuwa rasmi kiliundwa kwenye Ofisi yake, kwa  kutumia fedha za umma zinazokadiriwa kuwa Dola 950,000.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ripoti kutoka Ofisi ya rais Tinubu, zinasema uundwaji wa baraza la rais linayoshughulikia mambo ya nje, haikuwa halali licha ya kufikiriwa kuwa ilikuwa Idara kwenye Ofisi ya kiongozi huyo wa nchi.

Polisi wanasema wanamtafuta Adeniyi Adeyemi Matthew, ambaye amekuwa akidai kuongoza baraza hilo kwa kughushi nyaraka, na kujitambulisha kama mfanyakazi kwenye ofisi ya rais.

Kabla ya kutoweka kwake, Adeyemi, alisema alikuwa hana hatia na sasa anahofia maisha yake, licha ya kuahidi kusafisha jina lake Mahakamani.

Rais Tinubu, ameagiza Tume inayosimamia vita dhidi ya rushwa kuchunguza sakata hilo na kumpa ripoti ya kina ndani ya sikua 30.

Hatua hii imekuja baada ya wanasiasa wa upinzani na wanaharakati kushinikiza kuwepo kwa uchunguzi huru na wale wote waliohusika kuchukuliwa hatua za kisheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *