Yanga imemtambulisha kocha Manqoba Mngqithi kuwa kocha wao mpya akichukua nafasi ya Pedro Goncalves.

Manqoba ambaye ni kocha wa zamani wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha Yanga.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema kocha huyo ataanza kazi haraka ya kuandaa kikosi hicho tayari kwa msimu ujao.

Kocha huyo mwenye mafanikio makubwa nchini Afrika Kusini anatua Yanga ikitaka aipe mafanikio kwenye soka la Afrika.

Manqoba (56) anatua Yanga akitokea Golden Arrows ya Afrika Kusini, iliyomaliza nafasi ya sita msimu uliopita wa Ligi ya nchini humo.

Bado Yanga haijaweka wazi kuwa kocha huyo atatua nchini lini kuanza kazi hapa nchini kukiandaa kikosi cha Mabingwa hao.

Awali Yanga ilihusishwa na kocha Fadlu Davids lakini Mwanaspoti linafahamu kwamba pande hizo mbili zilishindwana mezani wakati wa makubaliano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *