Jeshi la Mali na washirika wake kutoka Urusi, Africa Corps wamepata mafanikio makubwa: msafara ulioondoka Gao mnamo Julai 7 uliwasili Anéfis jioni ya Julai 9 baada ya mapigano marefu na mabaya na waasi wa Azawad Liberation Front (FLA) wakishirikiana na wanajihadi wa JNIM.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi walioko Anéfis hatimaye wamepokea udaidizi wa wanajshi wengine waliokuwa wanasubiriwa na wanaimarisha udhibii wao katika eneo hili la kimkakati katikajimbo la Kidal. Hata hivyo, makundi yenye silaha hayakusudii kuishia hapo.

Baada ya mapigano ya saa kumi—ambayo pande zote mbili zinayaelezea kama “makali”—msafara huo hatimaye ulifika Anéfis jioni ya siku ya Alhamisi, Julai 9, karibu saa 2:00 usiku.

Msafara huo, ambao ulikabiliwa na hatari nyingi, ulifanikiwa kuwasili. baada ya kuepka mashambulizi ya wanajihadi wa JNIM na waasi wa Azawad Liberation Front (ALF) siku nzima lakini uliweza kupita kwa mafanikio makubwa. Makundi yenye silaha hatimaye yaliondoka, na kuacha mji na kambi ya kijeshi ya Anéfis mikononi mwa wanajeshi wa Mali na washirika wao wa Urusi kutoka Kikosi cha Africa Corps.

Vifo na majeraha vimeripotiwa pande zote mbili, na magari mengi ya kivita na malori ya mizigo yaliharibiwa. Pande zote mbili zilitoa picha za uharibifu kwa kila kambi hasimu, lakini hakuna takwimu za kuaminika za majeruhi zilizopatikana katika hatua hii.

Ndege za kivita na wapiganaji wa Tuareg

Ingawa maelezo ya mapigano yanatofautiana kulingana na unayezungumza naye, kila mtu anakubaliana kuhusu jambo moja: Ni ndeger za kivita zilizowawezesha wanajeshi wa Mali na washirika wao wa Urusi kupata ushindi. “Kwa kutumia ndege zisizo na rubani na ndege za Sukhoi, ilikuwa vigumu kwetu kupigana chini ya mashambulizi mengi,” alikiri afisa wa jeshi kutoka FLA. Uwepo ndani ya vikosi vya Mali vya wapiganaji wa Tuareg kutoka makundi ya kisiasa na kijeshi ya kaskazini yaliyoshirikiana na mamlaka – Gatia na MSA – pia ulichangia pakubwa. “Walikuwa wakikabiliana na watoto wa jangwani,” “wapiganaji wetu wanajua eneo lote kulikotokea mapigano hayo,” alisemai kiongozi na mwanachama wa makundi haya.

Kwa hivyo, dhamira imekamilika: kambi ya Anéfis inabaki mikononi mwa jeshi, na wanajeshi waliowekwa hapo hatimaye wameweza kupokea usaidizi unaohitajika sana wa wanajeshi na vifaa vya kijeshi. Usaidizi huu ulisubiriwa kwa hamu: siku ya Jumapili, Julai 5, msafara uliopita ulilazimishwa kurudi nyuma na makundi yenye silaha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *