Spain imeandika ukurasa mpya wa historia baada ya kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2026, ikiwa ni mara yao ya kwanza kufika hatua hiyo tangu mwaka 2010.
Mara ya mwisho Hispania ilifika nusu fainali ilikuwa Afrika Kusini mwaka 2010, walipoifunga Ujerumani kwa bao 1-0 kabla ya kuifunga Uholanzi fainali na kutwaa Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia yao.
Baada ya mafanikio hayo makubwa, Spain ilipitia kipindi kigumu kwenye michuano iliyofuata. Mwaka 2014 walitolewa hatua ya makundi, mwaka 2018 waliondolewa hatua ya 16 bora kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Urusi, huku mwaka 2022 wakitolewa tena hatua ya 16 bora baada ya kufungwa na Morocco kwa penalti.
Sasa, kizazi kipya cha wachezaji kimeirejesha Hispania kwenye ramani ya soka la dunia. Kwa ushindi wao dhidi ya Belgium katika robo fainali, Spain imefuzu nusu fainali kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 16 na inaendelea kuota ndoto ya kutwaa taji lao la pili la Kombe la Dunia.
Je, safari hii Spain itaandika historia nyingine kwa kutwaa ubingwa wa dunia tena

(Feed generated with FetchRSS)