
Marekani inataka Iran kutangaza hadharani kuwa eneo la mlango wa Hormuz limefunguliwa na kuahidi kuwa haitashambulia meli za mizigo zinazopita katika eneo hilo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wito huu umetolewa na maafisa wa Marekani ambao hawakutajwa kwa majina, ambao wameongeza kuwa, wawakilishi wa Iran wamekiri kwa washauri wa rais Donald Trump kuwa, kushambuliwa kwa meli katika eneo la la mlango wa Hormuz, lilikuwa kosa.
Haya yanajiri wakati huu wawakilishi wa Iran na Marekani wakitarajiwa kuendelea na majadiliano nchini Oman.
Rais Trump amesema licha ya nchi hizo mbili kushambuliana wiki hii, pande zote zimekubaliana kuendelea na mazungumzo yasiyokuwa ya moja kwa moja.
Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya nje wa Iran Abbas Araghchi, amesema nchi yake haitbadilisha msimamo wake, kuwa Marekani ndio ilivunja mkataba wa kusitisha vita.