
Seneta Lindsey Graham, anayetambuliwa kuwa mhandisi wa mipango ya Washington dhidi ya Iran na mhamasishaji mkuu wa Trump kufanya mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, hatimaye ameangamia na ndoto yake ya kunyakua “matrilioni ya dola katika pesa na mafuta ya Iran.”
Seneta huyo Mzayuni, ambaye mnamo Machi mwaka jana alitaja waziwazi lengo la vita vya Marekani dhidi ya Iran kuwa ni kuiba akiba ya nishati ya Iran, sasa amekwenda jongomeo na ndoto yake.
Graham alikuwa muungaji mkono mkubwa wa uvamizi wa Marekani nchini Iraq mwaka 2003 na kwa muda mrefu alikuwa akishinikiza vita dhidi ya Iran. Alikuwa muungaji mkono mkubwa wa utawala katili wa Israel na na mauaji ya kimbari ya utawala huo dhidi ya watu wa Palestina hususan katika Ukanda wa Gaza.
“Utawala wa Iran utakapoanguka, tutakuwa na Mashariki ya Kati mpya na tutapata mabilioni ya dola na hakuna mtu atakayetishia tena Lango-Bahari la Hormuz.” Hii ni sehemu ya matamshi ya Seneta Lindsey Graham katika mahojiano na Fox News mapema mwaka huu.
Jarida la Wall Street baadaye lilifichua kwamba alikuwa na nafasi muhimu katika kumshawishi Donald Trump kuanzisha shambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran.
Seneta Lindsey Graham ni mmoja wa waungaji mkono mashuhuri wa Marekani kwa Israel, wanaotaka utawala huo katili upewe kila kitu kinachohitajika ili “kushinda vita vyake” Ukanda wa Gaza.
Vilevile alipendekeza Israel ipewe ilaha za nyuklia ili kumaliza vita, sawa kabisa na Marekani ilivyoshambulia miji ya Hiroshima na Nagasaki ya Japani kwa mabomu ya nyuklia mwaka wa 1945, na akakosoa uamuzi wa Rais wa zamani wa Marekani, Joe Biden, wa kusimamisha baadhi ya shehena za silaha kwa jeshi la Israel.
Aliihimiza Israel kuendeleza mauaji ya watu wa Gaza wake, akihalalisha suala hilo kwa kusema kwamba “lazima ifanye kila linalowezekana kudumisha taifa la Kiyahudi.”
Seneta huyo wa chama cha Republican alifariki dunia Jumamosi jioni, Julai 11, 2026, baada ya kuugua ghafla na kwa muda mfupi.
Graham alikuwa amerejea Marekani hivi karibuni kutoka Ukraine, ambapo alikutana na Rais Volodymyr Zelenskyy kujadili uungaji mkono Washington kwa Kiev na vikwazo dhidi ya Urusi.