
Leo ni Jumatatu tarehe 28 Muharram 1448 Hijria inayosadifiana na tarehe 13 Julai 2026.
Siku kama ya leo miaka 1962 iliyopita, moto mkubwa ulitokea huko Roma mji mkuu wa utawala wa kifalme wa Roma.
Sehemu kubwa ya mji wa kihistoria na mkongwe wa Roma iliungua na wakazi wengi wa mji huo walipoteza maisha yao kutokana na moto huo.
Moto huo ulikuwa kisingizio tosha kwa Nuren mtawala mmwagadamu wa Kirumi ambaye aliwauwa kwa umati watu zaidi ya laki moja na baadaye kuwatuhumu Wakristo kuwa ndio walioanzisha moto huo. **
Katika siku kama ya leo miaka 792 iliyopita mji wa Baghdad uliokuwa makao makuu ya watawala wa Kiabbasi, ulitekwa na Hulagu Khan.
Hulagu alimuua mtawala al Muutasimu Billah na kukomesha kabisa utawala wa kizazi cha Bani Abbasi uliotawala maeneo mengi ya ulimwengu wa Kiislamu kwa kipindi cha miaka 500. Katika unyama huo mkubwa, Hulagu Khan alifanya ukatili mkubwa na kuua nusu ya watu wasiokuwa na hatia wa mji wa Baghdad.
Hulagu Khan pia alichoma moto nyumba na majengo mengi ya kihistoria ikiwemo maktaba kubwa ya Baghdad na idadi kubwa ya vitabu vyenye thamani kubwa vya maktaba hiyo viliteketea au kutumbukizwa katika mto Tigris. ****
Miaka 626 iliyopita katika siku kama ya leo, liliundwa jeshi la kale zaidi duniani nchini Uswisi.
Jeshi hilo la kale zaidi duniani hadi hii leo limebakia kama lilivyokuwa na hata mavazi ya wanajeshi wake hayajabadilika. Idadi ya wanajeshi wa jeshi hilo dogo lakini lenye nidhamu kubwa ni watu 83.
Jeshi hilo ambalo wanachama wake daima huwa raia wa Uswisi, liliundwa kwa ajili ya kulinda viongozi wa Kikatoliki wa wakati huo na hii leo baada ya kupita zaidi ya miaka zaidi ya 600 tangu liundwe, jeshi hilo lina jukumu la kumlinda Papa wa Kanisa Katoliki huko Vatican. ***
Katika siku kama ya leo miaka 255 iliyopita, baharia na nahodha mashuhuri wa Kiingereza aliyejulikana kwa jina la James Cook alikamilisha safari yake ya kitafiti na kielimu ya kuelekea The Great Southern Continent.
Safari hiyo ilikuwa imeanza tarehe 26 Julai mwaka 1768. Safari hiyo ndefu iliishirikisha pia timu ya watalaamu wa elimu ya Sayansi Asilia au Natural Science kwa kimombo.
Wataalamu hao walikuwa na nia ya kufanya utafiti wa kielimu kuhusiana na mimea pamoja na viumbe wanaopatikana katika maeneo hayo. ***
Katika siku kama hii ya leo miaka miwili iliyopita Muhammad Deif, mmoja wa makamanda mashuhuri wa kijeshi wa harakati ya Hamas na kamanda wa Brigedi za Izzuddin al-Qassam, aliuawa shahidi.
Muhammad Deif, ambaye jina lake halisi lilikuwa Muhammad Diab Ibrahim al-Masri, alizaliwa mwaka wa 1964 katika kambi ya wakimbizi ya Khan Yunis na baada ya kuvumilia kifungo kwa muda katika magereza ya Israel, alikuwa mmoja wa waanzilishi na makamanda wakuu wa Brigedi za Izzudd al-Qassam.
Kwa zaidi ya miongo mitatu, Muhammad Deif alichukua jukumu muhimu la kustawisha uwezo wa kijeshi wa Hamas, kubuni mtandao wa handaki za chini ya ardhi na kuimarisha uwezo wa makombora wa harakati hiyo ya mapambano ya ukombozi wa Palestina.
Muhammad Deif anajulikana kama mmoja wa wapangaji wakuu wa Operesheni “Kimbunga cha Al-Aqsa” na alinusurika majaribio kadhaa ya mauaji ya utawala wa Kizayuni wa Israel, ambayo yalipelekea ajulikane kama “Mtu Vivuli” au “Mtoto wa Kifo.”
Hatimaye Kamanda Muhammad al Deif aliuawa shahidi mnamo Julai 13, 2024, wakati wa shambulio la anga la Israel katika eneo la Khan Yunis. Muhammad Deif anatambuliwa kama mmoja wa makamanda wa kijeshi wenye ushawishi mkubwa na nembo ya mapambano dhidi ya uvamizi wa Israel.
Na tarehe 13 Julai inayosadifiana na Jumamosi ya leo ni siku ya kumbukumbu ya Romania kujipatia uhuru kutoka kwa Utawala wa Othmania. Kijiografia Romania ipo kusini mashariki mwa Ulaya na magharibi mwa Bahari Nyeusi. Romania ina zaidi ya wakazi milioni 22 na dini rasmi ya nchi hiyo ni Ukristo na madhehebu ya Orthodox ndiyo yenye wafuasi wengi. Nchi hiyo ilikuwa chini ya utawala wa Othmania kuanzia karne yay 15. Hata hivyo mwaka 1877 Romania iliungana na Russia katika vita dhidi ya utawala wa Othmania. Hatimaye katika siku kama ya leo Romalia ikajipatia uhuru na miaka mitatu baadaye ikawa imepata uhuru kamili.