Mamlaka za Luxembourg zimemfukuza kazi mwalimu wa shule ya msingia mbaye pia ni manusura wa mauaji ya halaiki ya Bosnia-Herzegovina baada ya kukosoa hadharani mauaji ya watoto katika Ukanda wa Ghaza kupitia machapisho yake kwenye mitandao ya kijamii.

Bi Fatima ameeleza wasiwasi wake kuhusu ukatili unaoendelea kufanywa na Israel katika eneo hilo la pwani lililoharibiwa na vita.

Akizungumza na vyombo vya habari, Fatima Kurtic amesema alifukuzwa kazi kwa sababu ameitetea Palestina na kupinga vita na mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya watu wa Gaza.

“Hakuna kinachoweza kunizuia kuizungumzia Palestina na yanayoendelea huko; watu wanauawa na kuteswa, mimi kama mwalimu na binadamu siwezi kukaa kimya mbele ya mauaji ya Gaza,” amesema mwalimu huyo wa shule ya msingi aliyefukuzwa kazi huko Luxembourg kwa kuitetea Palestina.

Wizara ya Elimu wa Luxembourg imesema kuwa uamuzi dhidi ya Fatima Kurtic ulifanywa kutokana na machapisho ambayo yametambuliwa kuwa ya chuki dhidi ya Wayahudi.

Bi Fatima Kurtic amepinga maelezo hayo, akisisitiza kuwa machapisho yake yanaukosoa utawala wa Israel na Uzayuni na si Wayahudi; na kwamba, siku zote amekuwa akipinga jinai za kivita na mauaji ya raia wasio na hatia.

Baada ya kufukuzwa kazi, wanafunzi, wazazi na waungaji mkono wake waliungana kuitisha maandamano ya amani wakitaka haki itendeke na kurejeshwa kazini mwalimu huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *