Wanaejeshi 30 wameuawa nchini Mali hivi karibni, katika vita vikali vya kudhibiti tena mji muhimu wa Anefis kutoka kwa kundi la kijihadi na waasi wa Tuareg.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi hao walipoteza maisha, katika makabiliano makali Ijumaa, baada ya mapigano ya karibu wiki moja, yaliyosababisha wao kuchukua tena mji wa Anefis.

Hata hivyo, mkuu wa majeshi Jean Elysee Dao, ametangaza kuuawa kwa wanajeshi hao akiongeza kuwa, wengine 60 wamejeruhiwa.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, waasi wa Tuareg walidai kuwauwa kwa idadi kubwa ya wanajeshi wa Mali na mamluki kutoka Urusi, katika Mji wa Anefis, uliopo umbali wa Kilomita 100 kutoka mji wa Kidal.

Tangu Julai tarehe 4, kundi la kijihadi la JNIM na waasi wa FLA, kutoka kabila la Tuareg, yamekuwa yakiendeleza mashambulizi ya kudhibiti Miji kadhaa ya Kaskazini mwa Mali  baada ya kudhibiti Kidal miezi kadhaa iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *