Jeshi la Marekani limetangaza kukamilisha awamu mpya ya mashambulio nchini Iran, ikisema hatua hiyo ililenga kuizuia Tehran kushambulia meli kwenye Mlango wa Bahari wa Hormuz.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Tangazo la Marekani limejiri baada ya wanajeshi wake kutekeleza mashambulizi mapya nchini Iran, wakati huu nchi hizo mbili zikiendelea kunga’ngani’a kudhibiti shughuli katika eneo la Bahari la Hormuz.
Kamandi ya jeshi la Marekani kupitia ukurasa wake wa kijamii wa X, imethibitisha kuwa imetekeleza mashambulizi 140 nchini Iran.
Rais Donald Trump anasema mashambulizi hayo, yanalenga kuhakikisha kuwa eneo la Bahari la Hormuz, linasalia wazi na kuruhusu kupita kwa meli za mizigo.
Kujibu mashambulizi hayo, jeshi la kulinda mapinduzi ya Iran, nalo limesema limelenga kambi za jeshi la Marekani nchini Jordan, Bahrain na Kuwait.
Aidha, Wizara ya Mambo ya nje ya Iran, imesema mashambulizi haya ya Marekani yamesababisha utovu wa usalama katika eneo la Bahari la Hormuz na kukwamisha safari za meli kwenda katika nchi mbalimbali.
Iran pia inasema mashambulizi haya, yanatatiza jitihada za hivi punde za kidiplomasia kupata mkataba wa kudumu.