
Donald Trump ametangaza siku ya Jumatatu, Julai 13, kwamba atarejesha kizuizi cha bandari za Iran na kutangaza nia yake ya kutoza ushuru kwa meli zinazotaka kupita kweye Mlango-Bahari wa Hormuz, njia ya majini ya kimkakati ambayo ndiyo kitovu cha makabiliano na Iran.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Tunarejesha ‘Kizuizi kwa bandari za Iran‘—kilichopewa jina hilo kwa sababu kinazuia tu meli au wateja wa Iran kuingia au kutoka,” rais wa Marekani alitangaza kwenye jukwaa lake la Truth Social.
Kama sehemu ya makubaliano ya amani kati ya Washington na Tehran, Marekani iliondoa kizuizi chake kwenye bandari za Iran mnamo Juni 18, kizuizi kilichowekwa miezi miwili mapema kujibu hautua ya Iran ya kufunga Mlango-Bahari wa Hormuz . Lakini kwa kuanza tena kwa uhasama kati ya nchi hizo mbili katika siku za hivi karibuni, rais wa Marekani alidai kwenye Fox News siku ya Jumatatu asubuhi, Julai 13, kwamba Marekani “itachukua udhibiti” wa mlango-bahari na kuwa “mlinzi” wake.
“Tutalipwa ili kulinda Mlango-Bahari wa Hormuz”
Marekani imekuwa ikilinda mlango huo “bure” hadi sasa, alidai, kabla ya kuongeza kwamba sasa italipwa fidia na mataifa mengine. “Tutalipwa ili kuulinda. Kiasi kikubwa; tunataka tu kulipwa kwa haya yote, kwa kuwaweka wanajeshi wetu katika hatari.”
Katika ujumbe kwenye Truth Social, rais wa Marekani alitaja kuanzishwa kwa kodi ambayo Marekani ingekusanya, sawa na “20% ya thamani ya shehena” ya meli zinazotaka kupitaa kwenye njia hiyo.
Iran inasisitiza kwamba njia ya Hormuz imefungwa hadi taarifa nyingine itakapotolewa kufuatia kuanza tena kwa mapigano makali ambayo hayajawahi kutokea tangu kusitishwa kwa mapigano mwezi Aprili katika mzozo wa Mashariki ya Kati. Njia hii ya kimkakati ya biashara ya hidrokaboni duniani ni jambo muhimu sana katika mzozo kati ya Washington na Tehran.
Donald Trump anakosoa mbinu za wapatanishi wa Iran
Donald Trump pia alilaani mbinu za wapatanishi wa Iran, ambao aliwashutumu kwa “kutokuwa na umuhimu wowote halisi” na kwa kupuuza ahadi zilizotolewa wakati wa mazungumzo yaliyofanyika siku iliyopita. “Jana, walifanya mkutano wa saa 11. (…) Kila kitu kilikuwa kimekubaliwa jana. Kisha wanatoka chumbani, wanapiga simu tena, na kusema wanapaswa kufanya mabadiliko,” aliongeza, bila kutaja aina ya mabadiliko hayo.
Kwa upande wake, diplomasia ya Iran inaishutumu Marekani kwa kuwajibika kwa “kurudi kwa ukosefu wa usalama” katika Mlango-Bahari wa Hormuz, ambapo sehemu ya tano ya mafuta ghafi duniani yalipitishwa hapo awali. Hata hivyo, Tehran ilidai siku ya Jumatatu kwamba ilikuwa ikiendelea na mashauriano na wapatanishi wa Qatar, Pakistai, na Oman ili “kuzuia hatari ya kuongezeka kwa uhasama huo.”