BAADA ya kuwepo na tetesi za kipa wa Mtibwa Sugar, Costantine Malimi kuhusishwa na Simba, taarifa mpya ni kwamba tayari JKT Tanzania imemfunga kwa mkataba wa miaka miwili utakaomalizika hadi  mwaka 2028.

Awali kipa huyo alikuwa kwenye rada za Simba lakini mwishoni Mwanaspoti likaripoti kuwa dili hilo limeshindikana baada ya kocha Steve Barker kutopitisha jina lake.

Chanzo cha ndani kutoka JKT Tanzania kilisema, baada ya Mtibwa kushuka daraja uongozi uliona ni rahisi kumpata Malimi wanayeamini ni kipa mzuri anaweza kuisaidia timu hiyo.

JK 01

Msimu uliyoisha Malimi alimaliza na ‘cleansheets’, anakwenda kumpa changamoto ya ushindani Omary Gonzo (cleansheets nne) na Ramadhani Chalamanda (cleansheets sita).

“Kila msimu Ligi Kuu inakuwa ngumu, hilo linatufanya kusajili na kuhakikisha kikosi kinakuwa imara chenye kuhimili ushindani wa hali ya juu,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

“Kuna wachezaji ambao wanaondoka pia, hivyo tutalazimika kusajili wengine wa kuziba pengo lao, lakini pia tumemuongezea mkataba kocha ili kuendelea kusalia na timu kwa msimu ujao.”

JK 02

Mchezaji mwingine kutoka Mtibwa anayetajwa kajiunga na JKT Tanzania ni kiungo mshambuliaji Ismail Mhesa aliyemaliza na mabao manne msimu uliyopita katika nafasi anayocheza kuna Valentino Mashaka (mabao sita), Paul Peter (mabao tisa) ambaye kulikuwa na taarifa za kufanya mazungumzo na timu ya nje.

Alipotafutwa Malimi kuhusiana na hilo amesema:”Sijui chochote kuhusiana na hicho unachokizungumza, JKT Tz hao ndio wenye jukumu la kutangaza wachezaji wao.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *