Rais wa Senegal Bassiroue Diomaye  Faye anatarajiwa  Ijumaa ,kukutana na mtangulizi wake Macky Sall ambaye anawania nafasi ya katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais huyo wa zamani amerejea nyumbani baada ya miaka miwili tangu kuondoka madarakani .

Ziara yake fupi inatarajiwa kuangazia namna Senegal itampa uungwaji mkono, Macky Sall ambaye amependekezwa na mwenyekiti wa  umoja wa Afrika Evariste Ndayishimiye kuwania nafasi hiyo.

Ujio wa Sally unatazamiwa kuwa na maana kubwa baada yake kujaribu kuahirisha uchaguzi ambapo aliondolewa madarakani.

Ndani ya chama cha Macky Sall,kuna imani kuwa ziara yake ni ziara tu kwa sababu uungwaji mkono w arais Faye tayari umehakikishwa.

Macky Sall alishindwa kupata uungwaji mkono wa pamoja wa Umoja wa Afrika baada ya nchi 20 ikiwemo Senegal kutumia turufu yake kuzuia kura hiyo.

Ofisi ya rais pamoja na chama cha Pastef hazijatoa taarifa zozote kuhusu ziara hiyo ya Ijummaa ,ila kwenye mitandao ya kijamii,wanaharakati tayari wameeleza kuchukizwa na ujio wa Macky Sall.

Watu 65 walipoteza maisha kwenye maandamano kati ya mwaka 2021 na 2023 wakati wa utawala wa Macky Sall.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *