.

Chanzo cha picha, Reuters

Iliyochapishwa

Muda wa kusoma: Dakika 3

Viktor Gyökeres anaweza kutumika kama sehemu ya makubaliano ya kumleta Julián Álvarez Arsenal, Liverpool imewasiliana na Paris Saint-Germain kuhusu Bradley Barcola, huku nahodha wa Tottenham, Cristian Romero, akitarajiwa kuondoka klabuni.

Arsenal inafuatilia uwezekano wa kumtoa mshambuliaji wa Uswidi, Viktor Gyökeres, 28, kama sehemu ya makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Argentina wa Atletico Madrid, Julián Álvarez, 26. (Talksport)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Barcelona itarejea katika mbio za kumsajili Álvarez baada ya Kombe la Dunia na huenda pia ikamjumuisha mmoja wa wachezaji wake katika makubaliano hayo. (Mundo Deportivo – in Spanish)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Barcelona wanataka kumpa mshambuliaji wa Hispania Ferran Torres, 26, mkataba mpya huku Paris Saint-Germain ikivutiwa naye lakini wanapanga kusubiri hadi Septemba kwa sababu ya kanuni za kifedha. (Mundo Deportivo)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Liverpool imeanzisha mawasiliano mapya na Paris Saint-Germain kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Bradley Barcola, 23, katika dirisha hili la usajili. (TeamTalk)

Arsenal inajaribu kumuuza mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus, huku AC Milan ikiwa miongoni mwa vilabu vinavyoongoza katika mbio za kutaka kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 29. (TeamTalk)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Sunderland ipo mbioni kukamilisha usajili wa beki wa kulia wa Ubelgiji Thomas Meunier kufuatia kuondoka kwake Lille. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 anatarajiwa kujiunga na klabu hiyo hivi karibuni. (Athletic – subscription required)

Liverpool imekataa ofa mpya ya Inter Milan kwa ajili ya Curtis Jones, huku dau lililoboreshwa la takriban pauni milioni 27 likishindwa kufikia kiasi cha pauni milioni 30 ambacho Liverpool inakitaka kwa kiungo huyo wa England mwenye umri wa miaka 25. (Talksport)

.

Chanzo cha picha, Rex Features

Everton imeongeza juhudi zake za muda mrefu za kumsajili beki wa kulia wa Genoa na timu ya taifa ya England chini ya miaka 21, Brooke Norton-Cuffy, baada ya kufanya mazungumzo mapya kuhusu uwezekano wa uhamisho wake. (TeamTalk)

Nahodha wa Tottenham Hotspur, Cristian Romero, 28, anatarajiwa kuondoka klabuni msimu huu wa joto, huku Barcelona ikionyesha nia ya kumsajili beki huyo wa kimataifa wa Argentina. (Talksport)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Mawakala wa Crysencio Summerville wamekutana na Roma kuhusu uwezekano wa mshambuliaji huyo wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 24 kujiunga nao akitokea West Ham. (Corriere dello Sport – in Italian)

Kipa wa Marekani Gabriel Slonina, 22, kwa sasa yuko kwenye majaribio na Strasbourg, huku kukiwa na uwezekano wa kuhamia huko akitokea Chelsea. (L’Equipe – in French)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *