
Jeshi la Iran leo Jumatano Julai 15, limezindua awamu ya nane ya operesheni yake ya “Saeqeh”, likilenga tena maeneo ya Marekani katika mashariki ya Kati.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na taarifa iliyotangazwa na televisheni ya taifa ya Iran IRIB, ndege zisizo na rubani zenye vilipuzi zilishambulia kambi ya anga ya Jordan ya Al-Azraq kwa mara ya pili, zikilenga ndege za kivita za F-18 na mahali pa kuhifadhia vyombo vya angani vya jeshi. Baadaye Jordan imetangaza kwamba imezuia makombora matatu ya balestiki ya Iran yaliyorushwa kuelekea eneo lake.
Siku ya nne ya mashambulizi ya anga ya Marekani dhidi ya Iran imeanza, huku Iran ikilipiza kisasi kwa kulenga maeneo ya kijeshi ya Marekani huko Kuwait, Bahrain, na Jordan. Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kimetishia kwamba “Mlango-Bahari wa Hormuz utaendelea kufungwa hadi mwisho wa uchokozi wa Marekani.” Wanadai kushambulia maghala, vituo vya mafuta, na kituo cha kamandi ya Kikosi cha Tano cha Marekani huko Bahrain. Vikosi vya kijeshi vya Jordan vilitangaza kuharibu makombora matatu ya balestiki ya Iran leo Jumatano asubuhi, yaliyofyatuliwa kuelekea kambi inayotumiwa na Marekani.
Hata hivyo, Donald Trump amewaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya White House kwamba makubaliano na Iran bado “yanawezekana.” Iran iliishutumu Marekani kwa “kuvunja” mkataba wa makubaliano uliolenga kukomesha vita, ikisema kwamba uamuzi wake wa kurejesha kizuizi cha bandari za Iran ulikuwa ukiukaji wa ahadi zake.