
Umoja wa Mataifa umesema viwango vya chanjo ya watoto wachanga duniani viliongezeka kidogo mwaka jana, lakini ukaonya kuwa kupunguzwa kwa ufadhili, migogoro na taarifa potofu kumesababisha kuongezeka kwa pengo la utoaji chanjo na kuruhusu milipuko kuongezeka.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa takwimu zilizochapishwa na shirika la afya duniani WHO na lile la watoto UNICEF, mwaka jana, asilimia 90 ya watoto wachanga duniani, walipata angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya dondakoo na pepopunda wakati asilimia 85 walikamilisha mfululizo wa dozi tatu.
Mashirika hayo yameonya kuwa idadi kubwa ya watoto katika nchi masikini huanza safari ya chanjo lakini hawamalizi dozi, mkuu wa UNICEF Catherine Russell, akisema kurejea kwa viwango vya chanjo duniani kunaficha ukweli kwamba mamilioni ya watoto wanaendelea kuachwa nyuma.
Katika ripoti yao, wamezungumzia mlipuko wa surua, ulioripotiwa katika nchi 57 mwaka jana, watoto wengi wakikosa chanjo kutokana na taarifa za uongo zinazotolewa kuhusu chanjo ya surua inayotolewa kati ya miezi 9 hadi 12.