Nchini Burkina Faso mamlaka imetoa saa 72 kwa wanadiplomasia wawili wa Umoja wa Ulaya kuondoka nchini humo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kupitia shirika la habari la AIB linalomilikiwa  na utawala wa kijeshi wanadiplomasia hao wametajwa kama watu wasiotakikana na kutakiwa kuondoka mara moja.

Wanadiplomasia wawili waliolengwa kupitia ujumbe huo ni naibu kiongozi wa ujumbe wa EU anayehusika na maswala ya siasa,habari na vyombo vya habari na meneja wa programu.

Utawala wa kijeshi haujatoa maelezo yoyote  kufafanua hatua hiyo ,ila inakuja baada ya hapo mwezi Juni  bunge la EU kupitisha  hoja iliyokosoa utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso kuminya uhuru wa raia kujieleza,kufanya ukamataji wa kiholela na kukithiri ukiukaji wa haki za binadaam nchini humo.

Kiongozi wa ujumbe wa EU awali aliagiziwa na waziri wa mambo ya nje wa Burkina faso aliyetaja hatua ya EU kama ukoloni wa kisasa na ukiukaji wa sheria kuhusu nchi zingine kuingilia maswala ya nchi nyingine.

Mjumbe maalum wa umoja huo ukanda wa Sahel aliyekuwa ziarani Burkina Faso ,wakati wa kutolewa amri hiyo ,anasema alishtushwa kuona miadi na mamlaka tofauti zikifutwa.

EU ikijibu hatua hiyo imesema imesikitishwa na hatua hiyo ikiahidi kutoa mwelekeo baada ya kutathmini kwa ukina maendeleo hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *