Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dkt  Kizza Besigye amewakataa mawakili walioteuliwa na mahakama kuu kumwakilisha kwenye kesi ya uhaini dhidi yake.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Besigya ameiambia mahakama kuu inayoketi Kampala kwamba yuko tayari kuendelea na mawakili wake aliowachagua na hatokubali kuwakilisha na mawakili waliopendekezwa na mahakama bila kuwa na habari  za kutosha kuwahusu na iwapo wanafaa kwa kesi hiyo.

Msimamo huu wa Besigye unaleta mkwamo kwenye kesi yake iliyoanza kuskilizwa siku ya Jumatatu wiki hii.

Kabla kuahirishwa kesi hiyo siku  ya Jumatatu ,mahakama ilikuwa imemtaka kuwachagua mawakili wengine ,kwa kuwa wakili wake Erias Lukwago alikamatwa mwezi uliopita na jeshi huku wakili mwingine raia wa Kenya,Martha Karua akizuiliwa kuingia nchini humo.

Jaji anayeongoza kuskilizwa kesi hiyo Emmanuel Baguma  amempa Besigye majuma mawili kutathmini uamuzi wake ,ila Besigye bado anahoji kwa nini serikali inanganganiza kumpa mawakili .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *