Mashambulio dhidi ya wapiga kura wakati wa uchaguzi mdogo katika eneo bunge la Ol Kalou katika mkoa wa kati nchini Kenya, yameibua hofu kuhusu hali ya usalama kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Watu waliokuwa na silaha walivamia vituo vya kupigia kura wakati wa uchaguzi huo ukiendelea, wakirusha mabomu ya machozi na kuwashambulia wapiga kura pamoja na waandishi wa habari.

Magari ya raia yalionekana yakiwa na watu wenye silaha huku wakiwatisha wananchi kuacha kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa eneo hilo.

Huu ni uchaguzi mdogo wa kwanza kufanyika katika eneo la Mlima Kenya tangu aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kuondolewa katika nafasi hiyo baada ya mvutano ulioibuka kati yake na Rais William Ruto.

Tukio hilo limeibua hofu kuhusu uwezekano wa kuongezeka kwa vurugu za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaonya kuwa hali hiyo inaweza kuzorota zaidi huku Rais William Ruto akijiandaa kuwania muhula wa pili katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Agosti 2027.

Kwa mujibu wa matokeo ya awali ,mgombea wa chama cha DCP cha kwake Gachagua, Sammy Kamau Ngotho ameibuka  mshindi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *