TAARIFA kutoka Singida Black Stars, zinabainisha kwamba, kiungo wa kati wa Yanga, Shekhani Khamis, tayari ameshaanza mazoezi na kikosi hicho alichojiunga nacho kwa mkopo wa msimu mmoja wa 2026-2027, hatua hiyo imekujaa baada ya kukosa nafasi kubwa ya kucheza kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu ya NBC.

Shekhani aliyezaliwa Agosti 19, 2002 (umri wa 23) alijiunga na Yanga Desemba 16, 2023 akitokea JKU ya Zanzibar. Katika nafasi aliyokuwa anacheza Yanga washindani wake waliyokuwa wanacheza mara kwa mara ni Mohamed Damaro, Duke Abuya na Mudathir Yahya.

Kwa Singida BS ushindani ambao atakutana nao wa namba ni dhidi ya Ahmed Pipino, Linda Mtange, Khalid Habib Idd ‘Gego’ huku Khalid Aucho ikielezwa hataendelea kukichezea kikosi hicho.

KIU 01

Ukiachana na Shekhan, mwingine aliyeanza mazoezi na Singida Black Stars baada ya kusajiliwa kwa mkataba wa miaka mitatu ni kipa Yona Amosi aliyetoka Pamba Jiji ambaye msimu wa 2025-2026 alimaliza akiwa na cleansheets nane za Ligi Kuu ya NBC na 2024-2025 alikuwa na cleansheets 11.

Singida Black Stars imezipiku Simba na Yanga ambazo tangu msimu uliopita zilikuwa zinahusishwa kuhitaji huduma ya kipa huyo, lakini hazikufanikiwa kumsajili. Amosi anakwenda kukutana na ushindani wa kipa mzawa Metacha Mnata aliyemaliza msimu wa 2025-2026 wa Ligi Kuu akiwa na cleansheets tano pia amewahi kuzitumikia timu mbalimbali za Ligi Kuu kama Yanga, Azam, Polisi Tanzania na Mbao, pia Taifa Stars.

Wakati huohuo, taarifa za mshambuliaji Jonathan Sowah raia wa Ghana kurejea Singida Black Stars akitangazwa kuitumikia timu hiyo kuanzia 2026 hadi 2029, zimepokewa vizuri na kocha wa kikosi hicho, Muhibu Kanu.

KIU 02

“Haimanishi kama ameshindwa kucheza Simba basi atashindwa kucheza Singida, sisi tuna utaratibu wetu wa kuishi na wachezaji, kurejea kwake kutaongeza idadi ya mabao maana anajua kukaa kwenye nafasi ya kufunga na anatumia nafasi,” amesema Kanu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *