Umoja wa mataifa umeonya kuwa nchi za Afrika Mashariki zinakabiliwa na mahitaji makubwa ya kibinadamu, huku takriban watu milioni 48.5 wakihitaji msaada wa dharura mwaka huu.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa afisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu missada ya  Kibinadamu, OCHA, hali hiyo inachangiwa na migogoro, watu kukimbia makwao, athari za mabadiliko ya hali ya hewa, milipuko ya magonjwa na uhaba wa chakula.

Aidha, OCHA inaonya kuwa bado kuna hatari kubwa ya ugonjwa wa Ebola kusambaa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hadi mataifa jirani.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa kali imeongezeka na kufikia milioni 40.5 katika robo ya pili ya mwaka,nchi zilizoathirika zaidi ni Sudan Kusini, Kenya, Sudan na Tanzania.

Kwa upande mwingine, mzozo wa Mashariki ya Kati umechangia kupanda kwa gharama za mafuta, usafiri na chakula, hali inayotatiza usambazaji na kuongeza shinikizo kwa uchumi wa mataifa yaliyo hatarini.

Wakati huo huo, athari za mabadiliko ya tabianchi zimewalazimu karibu watu elfu 13 nchini Burundi kuyahama makazi yao, huku idadi ya wakimbizi katika ukanda huo ikiongezeka na kufikia milioni sita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *